Isaiah 9:17-19


17 aKwa hiyo Bwana hatawafurahia vijana,
wala hatawahurumia yatima na wajane,
kwa kuwa kila mmoja wao hamchi Mungu, nao ni waovu,
na kila kinywa kinanena upotovu.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.


18 bHakika uovu huwaka kama moto;
huteketeza michongoma na miiba,
huwasha moto vichaka vya msituni,
hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi.

19 cKwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote
nchi itachomwa kwa moto,
nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto.
Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.
Copyright information for SwhKC